Swali: Kuna mtu alinuia kusafiri pamoja na familia yake ambapo wakapanda gari na kuanza safari. Kukaadhiniwa kwa ajili ya ´Aswr ilihali bado hawajatoka katika mji wao. Je, wafupishe swalah au wafanye nini? Wakifika huko wanakoenda wafupishe swalah kama Dhuhr, ´Aswr, Maghrib na ´Ishaa ule muda wataokuwa huko?
Jibu: Kuhusu sehemu ya kwanza ya swali ambapo wakati wa swalah ukiingia ilihali bado uko katika mji halafu ukaanza safari, basi inafaa kwako kuswali kwa kufupisha hata kama kumeadhiniwa ilihali bado uko katika mji wako. Kwa sababu kinachozingatiwa ni ule utekelezaji swalah na sio kuingia kwa wakati wake. Kinyume chake iwapo wakati umekuingilia na wewe uko safarini kisha ukafika katika mji wako, katika hali hii utatakiwa kuswali Rak´ah nne kikamilifu. Kwa hivyo kinachozingatiwa ni ule utekelezaji swalah.
Kuhusu kufupisha tunakariri na kusema kwa mara ya tatu ya kwamba lililo bora kwa msafiri asikusanye isipokuwa anapokuwa katika pirika nyingi za safari au akawa na haja ya kufanya hivo.
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (32) http://binothaimeen.net/content/728
- Imechapishwa: 26/11/2017
Swali: Kuna mtu alinuia kusafiri pamoja na familia yake ambapo wakapanda gari na kuanza safari. Kukaadhiniwa kwa ajili ya ´Aswr ilihali bado hawajatoka katika mji wao. Je, wafupishe swalah au wafanye nini? Wakifika huko wanakoenda wafupishe swalah kama Dhuhr, ´Aswr, Maghrib na ´Ishaa ule muda wataokuwa huko?
Jibu: Kuhusu sehemu ya kwanza ya swali ambapo wakati wa swalah ukiingia ilihali bado uko katika mji halafu ukaanza safari, basi inafaa kwako kuswali kwa kufupisha hata kama kumeadhiniwa ilihali bado uko katika mji wako. Kwa sababu kinachozingatiwa ni ule utekelezaji swalah na sio kuingia kwa wakati wake. Kinyume chake iwapo wakati umekuingilia na wewe uko safarini kisha ukafika katika mji wako, katika hali hii utatakiwa kuswali Rak´ah nne kikamilifu. Kwa hivyo kinachozingatiwa ni ule utekelezaji swalah.
Kuhusu kufupisha tunakariri na kusema kwa mara ya tatu ya kwamba lililo bora kwa msafiri asikusanye isipokuwa anapokuwa katika pirika nyingi za safari au akawa na haja ya kufanya hivo.
Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (32) http://binothaimeen.net/content/728
Imechapishwa: 26/11/2017
https://firqatunnajia.com/ibn-uthaymiyn-msafiri-kuanza-kufupisha-akiwa-katika-mji-wake/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)