Ibn ´Uthaymiyn kuhusu Tarawiyh Rak´ah 23

Itambulike kuwa Sunnah ya Makhaliyfah hawa inakuja baada ya Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´aalyhi wa sallam). Lau Sunnah ya Khaliyfah mmoja wapo itaenda kinyume na Sunnah ya Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´aalyhi wa sallam), basi kunahukumiwa kwanza Sunnah ya Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´aalyhi wa sallam) na si mwingine. Sunnah ya Makhaliyfah iko nyuma ya Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´aalyhi wa sallam).

Kulitokea mjadala kati ya wanafunzi wawili kuhusu swalah ya Tarawiyh. Mmoja wao akasema Sunnah ni kuswali Rak´ah 23 na yule mwingine akasema Sunnah ni kuswali Rak´ah 13 au 11. Yule wa kwanza akamwambia huyu wa pili kwamba hii ni Sunnah ya Khaliyfah ambaye ni ´Umar bin al-Khattwaab ya kuwa ni Rak´ah 23. Huyu anataka kwenda kinyume na Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´aalyhi wa sallam). Yule wa pili akasema kuwa Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´aalyhi wa sallam) ndio yenye kutangulizwa. Hili ni kama itakuwa imesihi kutoka kwa ´Umar kwamba ni Rak´ah 23. Kwa sababu kilichosihi kutoka kwa ´Umar kwa upokezi ulio sahihi zaidi ambao umepokea Maalik katika “al-Muwattwa´” alimwambia Tamiym ad-Daariy au na ´Ubayy bin Ka´b wawaswalishe watu Rak´ah 11 na si 23. Hili ndio lililosihi kutoka kwa ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh). Vovyote itavyokuwa hatuwezi kuitelekeza Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´aalyhi wa sallam) kwa Sunnah ya yeyote yule, sawa ikiwa ni Makhaliyfah au wengine. Kinachoenda kinyume na Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´aalyhi wa sallam) miongoni mwa Sunnah za Makhaliyfah wanapewa udhuru. Lakini hata hivyo hakitumiwi kama hoja kama ambavyo hakifanywi vilevile kuwa ni hoja juu ya Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´aalyhi wa sallam).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/283-284)
  • Imechapishwa: 06/11/2024