Swali: Baadhi ya Anaashid za Kiislamu zinaimbwa pamoja na ngoma. Zinapelekea katika hamasa na zinakuwa na maana nzuri. Ni yapi maoni yako?
Jibu: Kumekithiri maneno juu ya Anaashiyd za Kiislamu. Kumeshapita muda mrefu tangu nizisikie. Mara ya kwanza zilipotoka zilikuwa ziko sawa. Zilikuwa hazina ngoma. Zilikuwa hazipelekei katika fitina na wala haziimbwi kwa midundo ya haramu. Lakini muda ulivyozidi kwenda zimezidi kukuwa. Zikaanza kuchanganywa na midundo. Kuna uwezekano ikawa ni ngoma au kitu kingine. Baada ya hapo zikakuwa zaidi na kuanza kuimbwa kwa sauti nzuri na zenye kufitinisha. Baada ya hapo zikazidi kukuwa na kuanza kuimbwa kwa mtindo wa nyimbo zilizoharamishwa. Kwa ajili hiyo ndani ya nafsi yangu nahisi kitu. Mtu hawezi kusema kuwa zote zinafaa kwa hali yoyote kama ambavyo mtu hawezi kusema vilevile ya kwamba zote ni haramu kwa hali yoyote. Zitakuwa ni zenye kufaa ikiwa zitakuwa hazina yale mambo ambayo nimetoka kuyaashiria punde tu. Ama ikiwa zitaambatana na ngoma, sauti nzuri nzuri na zenye kufitinisha au zikaimbwa kwa midundo ya nyimbo, itakuwa haijuzu kuzisikiliza.
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (11)
- Imechapishwa: 03/05/2020
Swali: Baadhi ya Anaashid za Kiislamu zinaimbwa pamoja na ngoma. Zinapelekea katika hamasa na zinakuwa na maana nzuri. Ni yapi maoni yako?
Jibu: Kumekithiri maneno juu ya Anaashiyd za Kiislamu. Kumeshapita muda mrefu tangu nizisikie. Mara ya kwanza zilipotoka zilikuwa ziko sawa. Zilikuwa hazina ngoma. Zilikuwa hazipelekei katika fitina na wala haziimbwi kwa midundo ya haramu. Lakini muda ulivyozidi kwenda zimezidi kukuwa. Zikaanza kuchanganywa na midundo. Kuna uwezekano ikawa ni ngoma au kitu kingine. Baada ya hapo zikakuwa zaidi na kuanza kuimbwa kwa sauti nzuri na zenye kufitinisha. Baada ya hapo zikazidi kukuwa na kuanza kuimbwa kwa mtindo wa nyimbo zilizoharamishwa. Kwa ajili hiyo ndani ya nafsi yangu nahisi kitu. Mtu hawezi kusema kuwa zote zinafaa kwa hali yoyote kama ambavyo mtu hawezi kusema vilevile ya kwamba zote ni haramu kwa hali yoyote. Zitakuwa ni zenye kufaa ikiwa zitakuwa hazina yale mambo ambayo nimetoka kuyaashiria punde tu. Ama ikiwa zitaambatana na ngoma, sauti nzuri nzuri na zenye kufitinisha au zikaimbwa kwa midundo ya nyimbo, itakuwa haijuzu kuzisikiliza.
Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (11)
Imechapishwa: 03/05/2020
https://firqatunnajia.com/ibn-uthaymiyn-kuhusu-kukua-kwa-anaashiyd-%e2%80%82%e2%80%82/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)