Ibn Baaz kutumia Aayah za Qur-aan katika mazungumzo ya kawaida

Swali: Ni ipi hukumu ya kutumia baadhi ya matamshi au Aayah za Qur-aan katika mazungumzo ya kawaida, kama vile kumwambia mtu anapoingia nyumbani: ”Ingieni humo kwa salama mkiwa na amani” au kusema ”Umefika kwa wakati, ee Muusa” ikiwa mgeni anaitwa Muusa na maneno mengine kama hayo?

Jibu: Inavyoonekana haifai kutumia Qur-aan kama maneno ya kawaida ya mazungumzo au kama maneno ya kijamii. Haistahiki Qur-aan kufanywa kama nyenzo ya maongezi ya kawaida ya watu. Dunia si mahali pa salama kamili. Ndani yake kuna khofu, khatari na mauti. Mahali pa salama ya kweli ni Pepo. Allaah ndiye anayewalingania watu kwenye Nyumba ya salama, ambayo ni Pepo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1044/حكم-استعمال-بعض-الايات-مجرى-الكلام-العادي
  • Imechapishwa: 23/01/2026