Ibn Baaz kupita mbele ya anayeswali msikiti wa Makkah

Swali: Watu wengi wanachukulia wepesi katika kupita mbele ya anayeswali ndani ya msikiti wa Haraam na wanadai kwamba jambo hilo linajuzu katika msikiti huo kwa sababu ya msongamano na wala hawajitahidi kuliepuka. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Kinachojulikana kwa wanazuoni ni kuwa anayepita mbele ya anayeswali katika msikiti wa Haraam hazuiwi na wala si lazima kuweka Sutrah, kwa sababu mara nyingi kuna msongamano mkubwa na huwa ni vigumu kuweka Sutrah. Kwa hiyo asiyemzuia anayepita mbele yake, basi hapana vibaya juu yake – Allaah akitaka – katika hali kama hii kutokana na dharurah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/325)
  • Imechapishwa: 10/03/2026