Ibn Baaz kupeana mikono baada ya swalah II

Swali: Baadhi ya watu husalimiana kwa kushikana mikono na yule aliyeko kulia na kushoto baada ya kumaliza swalah. Baadhi yao husema: “Haraman”, jambo hili limeenea miongoni mwa waislamu na wanasema kwamba hakuna tatizo ndani yake?

Jibu: Waislamu wakikutana katika safu na wakasalimiana baadhi yao kwa baadhi au wakasalimiana baada ya swalah ya kujitolea na wakapeana mikono, basi yote hayo yamewekwa katika Shari´ah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Wanapokutana waislamu wawili ambapo wakapeana mikono, basi dhambi zao huanguka kama yanavyoanguka majani ya mti.”

Ama kama mmoja wao tayari alimsalimia mwenzake kabla ya kuanza swalah, basi hakuna haja ya kurudia salamu hiyo baada ya swalah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/314)
  • Imechapishwa: 09/03/2026