Ibn Baaz kuoa kwa nia ya kuacha III

Swali: Kuoa kwa nia ya kuacha?

Jibu: Kikosi kikubwa cha wanazuoni wanaona kuwa hapana vibaya. Hata hivyo bora ni kuacha kufanya hivo. Wanazuoni wengi wanaona kuwa hapana neno. Hilo ni jambo baina yake yeye na Mola wake. al-Awzaa´iy na wengineo wameonelea kuikataza. Bora ni kuacha kufanya hivo. Bora ni mtu asiweke nia hiyo. Hilo ndio bora na salama zaidi.

Swali: Baadhi ya watu wanasafiri kwenda katika baadhi ya miji kwa ajili ya nia hiyo?

Jibu: Haijalishi kitu. Bora ni kuepuka nia hiyo. Kuiacha ni salama zaidi kwa ajili ya kutoka nje ya makinzano.

Swali: Ndoa hiyo ni sahihi?

Jibu: Jopo kubwa la wanazuoni wanaona kufaa kufanya hivo. Hata hivyo bora zaidi ni kuacha hiyo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23903/ما-حكم-الزواج-بنية-الطلاق
  • Imechapishwa: 30/05/2024