Ibn Baaz kuhusu talaka zilizokatazwa na talaka tatu kwa mpigo

Swali: Je, talaka iliyoharamishwa inapita?

Jibu: Kama ilivyotangulia. Sahihi ni kuwa haipiti, ingawa kikosi kikubwa cha wanazuoni wanaona kuwa inapita. Lakini sahihi ni kuwa katika hedhi na nifasi haipiti kwa mujibu wa maoni yenye nguvu zaidi. Hayo ndio maoni sahihi. Jopo kubwa la wanazuoni wanaona kuwa inapita mtu akitaliki wakati wa hedhi au damu ya uzazi, talaka imepita.

Ama talaka ya mara tatu, inahesabiwa moja ikiwa imekuja kwa neno moja. Mfano aseme: ”Wewe nimekutaliki talaka tatu” au ”Yeye ametalikiwa mara tatu”, sahihi ni kwamba inahesabiwa moja.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30073/هل-يقع-الطلاق-المحرم-وطلاق-الثلاث-ام-لا
  • Imechapishwa: 05/09/2025