Ibn Baaz kuhusu Hadiyth za al-Bukhaariy na Muslim

Swali: Baadhi ya wanafunzi wanachukua minyororo ya wapokezi ya al-Bukhaariy na Muslim kwa ajili ya kuzisoma na kuzikosoa. Wanasema kwa mfano wanapotaja cheni ya al-Bukhaariy ya kwamba Hadiyth hii ni nzuri. Vivyo hivyo kuhusu Muslim.

Jibu: Maimamu wameafikina juu ya kuzikubali Hadiyth za ndani ya al-Bukhaariy na Muslim. Isipokuwa mambo machache ambayo al-Daraaqutwniy ameyakosoa ndani ya Muslim. Vinginevyo maimamu wameafikiana juu ya kukubali mapokezi ya al-Bukhaariy na Muslim na kwamba baada ya kuzidurusu na kuzipatiliza imebainika kusalimika kwake upande wa cheni zake. Watunzi wawili, al-Bukhaariy na Muslim, wamejitahidi katika hilo na kuzichagua kutoka katika mkusanyiko wa Hadiyth nyingi. Allaah awarehemu. Cheni zake ziko wazi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24617/هل-يوجد-خلاف-في-قبول-البخاري-ومسلم
  • Imechapishwa: 14/11/2024