Swali: Ni wakati gani mtu husema:
رَضيتُ باللَّهِ ربًّا، وبالإسلامِ دينًا، وبِمُحمَّدٍ رسولًا
”Nimeridhia Allaah kuwa Mola, Muhammad kuwa Mtume na Uislamu kuwa ndio dini yangu.”
Je, ni baada ya shahaadah mbili?
Jibu: Husema wakati wa shahaadah mbili:

Husema hivyo wakati wa shahaadah mbili katika adhaana. Sa´d bin Abiy Waqqaas kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Atakayesema wakati muadhini anaposema: ”Nashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah:

”Nimeridhia Allaah kuwa Mola, Muhammad kuwa Mtume na Uislamu kuwa ndio dini yangu.”,
basi atasamehewa dhambi zake.”
Husema hivyo wakati wa shahaadah mbili katika adhaana na katika Iqaamah.
Swali: Je, mtu anamswalia Mtume kabla ya du´aa inayosema:
اللَّهُمَّ ربَّ هَذه الدَّعْوَةِ التَّامَّةِ والصَّلاَةِ الْقَائِمَةِ آتِ مُحَمَّداً الوسيلة والْفَضِيلَةَ وَابْعَثْهُ مَقَاماً محموداً الذي وَعَدْتَهُ
“Ee Allaah, Mola wa mwito huu uliotimia na swalah iliosimama! Mpe Muhammad Njia (الوسيلة) na fadhilah, na mfikishe daraja yenye kusifiwa ambayo umemuahidi.”?
Jibu: Ndio, hiyo ndiyo Sunnah. Amswalie Mtume kisha aombe du´aa hiyo.
Swali: Hilo ni kwa ujumla wa dalili au kuna dalili maalum juu ya hilo?
Jibu: Ni kwa Hadiyth uliyosikia. Hadiyth ya ´Abdullaah bin ´Amr aliyoipokea Muslim katika ”as-Swahiyh” yake ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mtapomsikia muadhini basi semeni kama anavosema, kisha niswalieni. Kwani hakika mwenye kuniswalia mara moja, basi Allaah atamsifu mara kumi. Kisha niombeeni kwa Allaah Njia (الوسيلة), hakika hiyo ni ngazi Peponi. Haimstahikii isipokuwa mja miongoni mwa waja wa Allaah na nataraji mimi ndiye mwenye kuistahiki. Kwa hivyo mwenye kuniombea kwa Allaah Njia basi utamstahikia uombezi wangu.”[1]
Hivyo anamswalia Mtume kwanza kisha anasema:

“Ee Allaah, Mola wa mwito huu uliotimia na swalah iliosimama! Mpe Muhammad Njia (الوسيلة) na fadhilah, na mfikishe daraja yenye kusifiwa ambayo umemuahidi.”
Swali: Je, ni bora kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa namna anavyoswaliwa katika Tashahhud?
Jibu: Ndio, hilo ndilo bora zaidi. Kwa sababu amesema:
”Kisha niswalieni.”
Maana yake ni ile swalah aliyofundisha:
اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَعَلَى آلِ مُحَمَّدٍ، كَمَا صَلَّيْتَ عَلَى آلِ إِبْرَاهِيمَ، إِنَّكَ حَمِيدٌ مَجِيدٌ، اللَّهُمَّ بَارِكْ عَلَى مُحَمَّدٍ وَعَلَى آلِ مُحَمَّدٍ، كَمَا بَارَكْتَ عَلَى آلِ إِبْرَاهِيمَ، إِنَّكَ حَمِيدٌ مَجِيدٌ
“Ee Allaah! Msifu Muhammad, jamaa zake Muhammad kama Ulivyowasifu jamaa zake Ibraahiym. Kwani hakika Wewe ni Mwenye kuhidimiwa na Mwenye kutukuzwa. Ee Allaah! Mbariki Muhammad, jamaa zake Muhammad kama Ulivyowabariki jamaa zake Ibraahiym. Kwani hakika Wewe ni Mwenye kuhidimiwa na Mwenye kutukuzwa.”[2]
Iwapo atapunguza na akasema:
اللهم صلِّ وسلم على رسول الله
”Ee Allaah! Msifu na msalimie Mtume wa Allaah.”
kwa sababu fulani, tunataraji hakuna tatizo. Lakini kuleta swalah kamili ndilo bora zaidi.
Baadhi ya watu huongeza neno ´ngazi ya juu` (الدرجة الرفيعة), jambo ambalo ni kosa. Kwa sababu halimo katika mapokezi. Daraja ya juu ndiyo al-Wasiylah yenyewe. Ni makosa ya baadhi ya waandishi. Upokezi sahihi ni:

Swali: Lakini imetajwa katika baadhi ya mapokezi?
Jibu: Hilo ni kosa, kosa lililotokana na baadhi ya waandishi na wapokezi. Halimo katika mapokezi.
Swali: Kuna msemaji anayedai kwamba muadhini anaposema katika adhaana ya Fajr:
الصلاة خير من النوم
”Swalah ni bora kuliko usingizi.”
Mwitikiaji anatakiwa kusema:
لا حول ولا قوة إلا بالله
”Hapana nguvu wala namna isipokuwa kwa msaada Wako.”
Jibu: Hapana, hilo halina msingi. Unatakiwa kusema:
الصلاة خير من النوم
”Swalah ni bora kuliko usingizi.”
Kusema:

husemwa wakati muadhini anaposema:
حي على الصلاة، حي على الفلاح
”Njooni katika swalah! Njooni katika mafanikio!”
Ama wakati anaposema:
الصلاة خير من النوم
”Swalah ni bora kuliko usingizi.”,
unasema kama yeye.
Swali: Vipi kuhusu kuongeza maneno:
إنك لا تخلف الميعاد
”Hakika wewe huvunji ahadi.”?
Jibu: Hilo halina tatizo.
[1] Muslim (384).
[2] al-Bukhaariy (3370) na Muslim (406).
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31569/ما-الصيغ-الصحيحة-لادعية-الاذان-والترديد-معه
- Imechapishwa: 10/11/2025

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31569/ما-الصيغ-الصحيحة-لادعية-الاذان-والترديد-معه
Imechapishwa: 10/11/2025
https://firqatunnajia.com/ibn-baaz-akijibu-baadhi-ya-maswali-wakati-wa-kumuitikia-muadhini/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket