Ibn Baaz akijibu baadhi ya maswali kuhusu michezo ya watoto yenye umbo la vinyago vyenye sura

Swali: Vipi kuhusu michezo ya watoto iliyo katika umbo la vinyago vyenye sura?

Jibu: Kuna maoni tofauti kuhus michezo ya watoto. Baadhi ya wanazuoni wanaona hakuna tatizo nayo, kwa sababu imesimuliwa kuwa ´Aaishah alikuwa na baadhi ya vinyago. Lakini tahadhari ni kuacha jambo hilo. Ni bora zaidi kuondoa kila aina ya picha, ni mamoja iwe ni ya vinyago au vinginevyo.

Swali: Imekuja katika Hadiyth:

“… isipokuwa alama kwenye nguo”?

Jibu: Hiyo inamaanisha michoro na mapambo, si sura kamili.

Swali: Vipi picha zilizoko katika mavazi ya watoto?

Jibu: Hazifai.

Swali: Vipi kuhusu picha za TV?

Jibu: Hizo si picha za kudumu. Ni picha zinazoonekana kwa muda tu, si za kudumu.

Swali: Lakini zikihifadhiwa kwenye kanda ya video kwa mfumo wa picha?

Jibu: Ikiwa zinaweza kuonekana, haijuzu. Lakini kama haziwezi kuonekana, hakuna tatizo.

Swali: Zikiweza kuonekana kwenye skrini na video?

Jibu: Hizo hazihesabiki kuwa picha, kwa kuwa hazipo kwenye nguo, wala vazi, wala karatasi, wala kitu kingine cha kudumu, basi hakuna tatizo.

Swali: Ni lini inakuwa haramu?

Jibu: Ikiwa ni kwa ulazima unaojulikana kuwa ni wa dharurah, basi hakuna tatizo. Lakini kama si kwa dharurah, basi haifai kupiga picha.

Swali: Je, picha za kwenye TV si za viumbe vyenye roho?

Jibu: Allaah ndiye anajua zaidi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31584/هل-تدخل-صور-والعاب-الاطفال-في-المنهي-عنها
  • Imechapishwa: 10/11/2025