Swali: Je, inaruhusiwa kufupisha swalah na kuikusanya kwa mtu ambaye hali yake ni kusafiri mara kwa mara kutoka katika nchi yake kwenda nje yake, au kutoka mji mmoja kwenda mwingine, katika miji ambayo msafiri anaruhusiwa kufupisha na kukusanya swalah, kama madereva wa magari na wale walio katika hukumu yao kama wauzaji na wanunuzi wanaozunguka?
Jibu: Hawa wako katika hukumu ya wasafiri. Kwa hiyo imesuniwa kwao kufupisha swalah. Inajuzu pia kukusanya swalah kama wasafiri wengine kwa mujibu wa maoni ya wanazuoni wengi, kwa sababu ya ujumla wa dalili za Kishari´ah katika hilo. Hatufahamu dalili yoyote inayopinga jambo hilo. Ama kuhusu maneno ya baadhi ya wanazuoni kwamba msafiri ambaye yuko pamoja na familia yake na hakusudii kukaa katika mji maalum haruhusiwi kutumia ruhusa za safari ni maneno dhaifu ambayo hatujui yana msingi gani katika Shari´ah. Jambo hili limeelezwa pia na Abu Muhammad Ibn-ul-Qudamah (Rahimahu Allaah) katika ”al-Mughniy”.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/191)
- Imechapishwa: 10/03/2026
Swali: Je, inaruhusiwa kufupisha swalah na kuikusanya kwa mtu ambaye hali yake ni kusafiri mara kwa mara kutoka katika nchi yake kwenda nje yake, au kutoka mji mmoja kwenda mwingine, katika miji ambayo msafiri anaruhusiwa kufupisha na kukusanya swalah, kama madereva wa magari na wale walio katika hukumu yao kama wauzaji na wanunuzi wanaozunguka?
Jibu: Hawa wako katika hukumu ya wasafiri. Kwa hiyo imesuniwa kwao kufupisha swalah. Inajuzu pia kukusanya swalah kama wasafiri wengine kwa mujibu wa maoni ya wanazuoni wengi, kwa sababu ya ujumla wa dalili za Kishari´ah katika hilo. Hatufahamu dalili yoyote inayopinga jambo hilo. Ama kuhusu maneno ya baadhi ya wanazuoni kwamba msafiri ambaye yuko pamoja na familia yake na hakusudii kukaa katika mji maalum haruhusiwi kutumia ruhusa za safari ni maneno dhaifu ambayo hatujui yana msingi gani katika Shari´ah. Jambo hili limeelezwa pia na Abu Muhammad Ibn-ul-Qudamah (Rahimahu Allaah) katika ”al-Mughniy”.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/191)
Imechapishwa: 10/03/2026
https://firqatunnajia.com/hukumu-za-safari-kwa-ambaye-anasafiri-mara-kwa-mara/