Hukumu ya walinganizi wanaonyamazia mambo ya shirki na kufuru

Swali: Wanachuoni walioko katika miji ya Kiislamu ambao wanawaona waabudu makaburi  na wanawanyamazia juu ya Tawassul zao kwa asiyekuwa Allaah. Je, hawa ni wabaya zaidi kuliko wale ambao wanamchezea shere Allaah?

Jibu: Hili linahitajia upambanuzi. Ikiwa wanaamini kuwa kitendo hicho kinafaa wanakufuru. Ama ikiwa wanachukulia wepesi tu na hawakatazi maovu, lakini wao wenyewe hawakufanya na wala hawakuyaamini basi hayo ni mapungufu wanayofanya katika jambo la kuamrisha mema na kukataza maovu. Ama ikiwa wamecha kufanya hivo kwa sababu ya kuogopa kama wale ambao walikuwa Makkah na hawakuweza kukataza maovu kwa sababu ya kuwaogopa washirikina ni wenye kupewa udhuru.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-is-Shubuhaat, uk. 131