Hukumu ya kuathiri ndoa kwa njia mbaya

Swali: Ni ipi hukumu kwa mtu ambaye anaathiri maisha ya ndoa ya mume na mke kwa njia mbaya? Mtu huyo ni katika jamaa wa karibu na mke.

Jibu: Ni haramu kumuharibia mwanamke kwa mume wake sawa bila kujali mwenye kufanya hivyo ni ndugu au sio ndugu. an-Nasaa´iy, Abu Daawuud na Ibn Hibbaan wamepokea kupitia kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kumuharibia mwanamke kwa mume wake sio katika sisi.”

Imepokewa na Abu Daawuud.

Check Also

Pato la haramu kwa shangazi mgonjwa na muhitajiaji

Swali: Nilipata mali kwa njia ya haramu. Je, inajuzu kumpa nazo shangazi yangu ambaye ni …