Hiyo ni bishara ya haraka kwa muumini

Swali: Vipi kwa mtu anayefurahia sifa za watu juu yake?

Jibu: Halimdhuru ikiwa hakufanya kwa ajili yao. Kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Hiyo ni bishara ya haraka kwa muumini.”

Ikiwa amefurahi kwa kusifiwa lakini hakufanya kwa ajili yao, bali wamesikia kuwa analingania kwa Allaah ambapo wakamuombea du´aa na kumsifia, au wamesikia kuwa anatoa swadaqah wakamuombea du´aa na kumsifia, ilihali yeye hakuwakusudia, basi halimdhuru. Hiyo ni bishara ya haraka kwa muumini.

Swali: Vipi maneno ya anayesema kuwa alama ya kumtakasia nia Allaah ni mtu kuwa sawa kwake kusifiwa na kusemwa vibaya?

Jibu: Hapana, si sharti. Ikiwa atafurahi kwa maombi mazuri ya watu, halimdhuru. Hiyo ni bishara ya haraka kwa muumini.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31131/هل-يتنافى-الاخلاص-مع-السرور-بثناء-الناس
  • Imechapishwa: 04/10/2025