Swali: Ni yepi maoni sahihi ikiwa hirizi ni ya Qur-aan?

Jibu: Imekatazwa. Ni mamoja hirizi ni ya Qur-aan au isiyokuwa ya Qu-aan maoni sahihi ni kwamba imekatazwa.

Swali: Lakini hirizi ikiwa ya Qur-aan inafikia katika kiwango cha shirki kubwa?

Jibu: Ni shirki ndogo. Ni kwa sababu ni njia [inayopelekea katika shirki kubwa] na ni kwa ajili ya kuenea kwa dalili.

Swali: Je, inakuwa kufuru kubwa mtu akiamini kuwa inanufaisha na kudhuru?

Jibu: Ni kufuru kubwa akiamini kuwa yenyewe kwa dhati yake ndio inanufaisha na kudhuru.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22398/حكم-التميمة-اذا-كانت-من-القران
  • Imechapishwa: 18/03/2023