Swali: Ni ipi hukumu ya mwanamke kuvaa mavazi meupe?

Jibu: Msingi wake ni kujuzu ikiwa si kwa mtindo wa mavazi ya wanaume. Lakini kwa vile mara nyingi vazi hilo linavaliwa na wanaume bora ni kuliepuka. Kwa ajili hiyo anakatazwa kufanya hivo kutokana na sababu hiyo, kwa sababu mara nyingi anakuwa amejifananisha kidhahiri na wanaume. Wanaume ndio mara nyingi huvaa mavazi meupe. Lakini akivaa kwa njia maalum inayohusu wanawake si kujifananisha. Ni kama vile wao ndio wamezowea kuvaa mavazi mekundu, kijani na meusi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24814/حكم-لبس-البياض-للنساء
  • Imechapishwa: 13/12/2024