Muulizaji swali ni Abul-Fadhwl Qaasim Mafuta:
Pindi tunapowasimamishia hoja Suruuriyyuun kuhusu aliyoyasema Sayyid Qutwub na kwamba anazungumza kwa imani ya kwamba Allaah yuko kila mahali na mengneyo ambayo wanachuoni wameandika juu yake na kwamba anawatukana Mitume, anamtukana ´Uthmaan bin ´Affaan (Radhya Allaahu ´anh) na mengineyo tele, wao wanatumia hoja juu ya uombezi wa Shaykh Ibn Baaz…
Rabiy´ al-Madkhaliy akijibu:
Shaykh Ibn Baaz hakumsoma mtu huyu. Lau angelitakaswa na watu milioni moja mfano wa Ibn Baaz na ilihali vitabu vyake vinatoa ushuhuda dhidi yake juu ya upotevu wake, matakaso ya wengine yasingelimfaa chochote. Hili ni kwa sababu yule msifiaji amejengea juu ya dhahiri. Shaykh Ibn Baaz alitegemea porojo za al-Ikhwaan al-Muslimuun juu ya Sayyid Qutwub. Pindi aliposoma baadhi ya maneno yake akasema kuwa ni maneno machafu. Aliposoma baadhi ya maneno yake kwa mfano aliyosema kuhusu Mu´aawiyah na ´Amr [bin al-´Aasw], akasema kuwa ni maneno machafu. Alipoulizwa kuhusu kitabu kilichoandikwa haya akasema kichanwe na kuraruliwa. Ibn Baaz hakumsoma. Yeye mwenyewe alisema kuwa hakusoma vitabu vya Sayyid Qutwub. Alisomewa aliyoyasema kuhusu Muusa (´alayhis-Swalaatu was-Salaam) ambapo akasema kuwa ni kuritadi. Waraddini kwa kuwaambia haya. Vilevile haya yamenukuliwa kutoka kwa Shaykh Ibn Baaz. Kuna mkanda wake utafuteni na muuchukue. Amesema kuwa maneno yake ni machafu ambapo amemtukana Mu´aawiyah na ´Amr bin al-´Aasw (Radhiya Allaahu ´anhumaa). Amesema kuwa walikuwa wanasifika kwa uongo, khiyana, ghushi, unafiki, rushwa na matusi mengineyo. Amesema kuwa ni maneno machafu. Kadhalika akasema kuwa kitabu hiki kichanwe na kuraruliwa. Pindi aliposikia baadhi ya matusi yake kumtukana Muusa (´alayhis-Swalaatu was-Salaam) akasema kuwa ni kuritadi.
Mosi ni kuwa Ibn Baaz hakumsoma. Pindi alipokuwa akiona kitu katika maneno yake anaonelea kuwa ni mpotevu na anahukumu maneno yake kuwa ni kuritadi ikiwa yanapelekea katika hilo.
Pili lau tutachukulia kuwa Ibn Baaz alimtetea na hakupatapo kuzungumza dhidi yake kabisa, hii sio hoja kwake. Ukosoaji uliofafanuliwa unatangulizwa juu ya usifiaji wa kijumla. Pamoja na kuwa Sayyid Qutwub hakusifiwa.
- Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: soundcloud.com/user-621373875/4-sheikh-rabii-ibn-haad-almadkhal
- Imechapishwa: 04/09/2020

Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: soundcloud.com/user-621373875/4-sheikh-rabii-ibn-haad-almadkhal
Imechapishwa: 04/09/2020
https://firqatunnajia.com/hata-wangekuja-ibn-baaz-milioni-wasingemtakasa-sayyid-qutwub/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)