Kuhusu talaka wakati wa ghadhabu inahitaji maelezo. Ghadhabu iko katika aina tatu:
1 – Ghadhabu ya kawaida. Ghadhabu aina hiyo haizuii talaka kupita.
2 – Ghadhabu kali inayobadilisha hali ya mtu na nia yake, kiasi kwamba hawezi kutoa talaka ya Kishari´ah, bali nia yake inafunikwa na njia yake inapotea kutokana na ugomvi mkali, mivutano, kupigana, kutukanana na matusi. Ghadhabu hii ikizidi, talaka aina hii haipiti pia kwa mujibu wa maoni sahihi.
3 – Ghadhabu inayomfanya mtu apoteze fahamu kabisa, awe kama watu walioondokewa na akili au wenye upungufu wa akili, kiasi kwamba haelewi anachokisema. Huyu talaka yake haipiti kwa makubaliano ya wanazuoni wote. Katika hali hii anazingatiwa pamoja na watu wasio na akili timamu. Talaka yake haipiit ikiwa ghadhabu imemfikisha katika hali hii.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2195/حكم-الطلاق-ثلاثا-بلفظ-واحد
- Imechapishwa: 04/03/2026
Kuhusu talaka wakati wa ghadhabu inahitaji maelezo. Ghadhabu iko katika aina tatu:
1 – Ghadhabu ya kawaida. Ghadhabu aina hiyo haizuii talaka kupita.
2 – Ghadhabu kali inayobadilisha hali ya mtu na nia yake, kiasi kwamba hawezi kutoa talaka ya Kishari´ah, bali nia yake inafunikwa na njia yake inapotea kutokana na ugomvi mkali, mivutano, kupigana, kutukanana na matusi. Ghadhabu hii ikizidi, talaka aina hii haipiti pia kwa mujibu wa maoni sahihi.
3 – Ghadhabu inayomfanya mtu apoteze fahamu kabisa, awe kama watu walioondokewa na akili au wenye upungufu wa akili, kiasi kwamba haelewi anachokisema. Huyu talaka yake haipiti kwa makubaliano ya wanazuoni wote. Katika hali hii anazingatiwa pamoja na watu wasio na akili timamu. Talaka yake haipiit ikiwa ghadhabu imemfikisha katika hali hii.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2195/حكم-الطلاق-ثلاثا-بلفظ-واحد
Imechapishwa: 04/03/2026
https://firqatunnajia.com/hasira-aina-tatu-wakati-wa-talaka/