Swali: Inajuzu kuwapa makafiri mafukara kondoo aliyekufa mwenyewe?

Jibu:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَنفِقُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا كَسَبْتُمْ وَمِمَّا أَخْرَجْنَا لَكُم مِّنَ الْأَرْضِ ۖ وَلَا تَيَمَّمُوا الْخَبِيثَ مِنْهُ تُنفِقُونَ وَلَسْتُم بِآخِذِيهِ إِلَّا أَن تُغْمِضُوا فِيهِ

“Enyi mlioamini! Toeni katika vizuri mlivyochuma na katika ambayo Tumekutoleeni kutoka katika ardhi na wala msikusudie vibaya kutoka humo mkavitoa na hali nyinyi wenyewe si wenye kuvichukuwa isipokuwa kwa kuvifumbia macho.” (02:267)

Hiki si kwamba ni kichafu tu, bali ni haramu. Hiki si kwamba ni kibaya tu, bali ni haramu. Haijuzu kutoa swadaqah kwa kitu haramu, si kumpa kafiri wala muislamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (03) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/omdah–14340316.mp3
  • Imechapishwa: 25/08/2020