Hapa ndipo unaweza kufunga siku sita za Shawwaal

Swali: Unasemaje kwa yule ambaye anafunga siku sita za Shawwaal ilihali yuko na deni la Ramadhaan?

Jibu: Jibu linapatikana katika maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Atakayefunga Ramadhaan kisha akaifuatishia siku sita za Shawwaal basi ni kama ambaye amefunga mwaka mzima.”

Yule mwenye deni la Ramadhaan akifunga siku sita za Shawwaal hazingatiwi kuwa ameifunga Ramadhaan kisha akaifuatishia siku sita za Shawwaal. Hazingatiwi kuwa ameifunga Ramadhaan isipokuwa baada ya kuikamilisha. Kwa hivyo halipwi kufunga siku sita za Shawwaal kwa yule aliyefunga siku hizo ilihali yuko na deni la Ramadhaan isipokuwa mpaka pale atakapoifunga Ramadhaan kisha ndio akafunga siku hizo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (20/19-20)
  • Imechapishwa: 08/06/2019