Hapa ndipo madhambi hubadilishwa kuwa mema

Swali: Ni lini madhambi hubadilishwa kuwa mema?

Jibu: Hubadilishwa kuwa mema pale mtu anapotubu na akafanya matendo mema, kama alivyoeleza Allaah:

إِلَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ عَمَلًا صَالِحًا

“Isipokuwa [hatoadhibiwa] yule aliyetubu na akaamini na akatenda matendo mema.”[1]

Swali: Je, tawbah ya kweli hubadilisha madhambi kuwa mema?

Jibu: Ndio, hubadilishwa. Kama ilivyo katika Aayah Tukufu ya Suurah al-Furqaan. Mtu akitubu na kufanya matendo mema, Allaah hubadilisha kila dhambi aliyofanya kuwa mema. Kama Alivyosema:

وَإِنِّي لَغَفَّارٌ لِّمَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا ثُمَّ اهْتَدَىٰ

“Hakika Mimi ni Mwingi wa kusamehe kwa anayetubia na akaamini na akatenda mema kisha akanyooka barabara.”[2]

إِلَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ عَمَلًا صَالِحًا

“Isipokuwa [hatoadhibiwa] yule aliyetubu na akaamini na akatenda matendo mema.”

Kwa maana ya kwamba ameongeza juu ya tawbah matendo mema ili kufidia yaliyopita.

[1] 25:70

[2] 20:82

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31135/هل-التوبة-الصادقة-تبدل-السيىات-حسنات
  • Imechapishwa: 04/10/2025