Hapa ndipo italazimu kufuata fatwa ya mwanachuoni

Swali: Katika kila nchi ya waislamu kuna Muftiy rasmi. Hivyo basi, ni lini fatwa ya Muftiy rasmi inakuwa yenye kuwalazimu watu kiasi cha kwamba haijuzu kwenda kinyume nayo?

Jibu: Fatwa rasmi au nyingine yoyote si ya lazima kufuatwa. Linalowalazimu watu ni maneno ya Allaah na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ikiwa Muftiy au mwanachuoni atatoa fatwa inayopingana na Shari´ah, basi fatwa hiyo si lazima. Yanayozingatiwa ni maneno ya Allaah na ya Mtume; Qur-aan na Sunnah. Ama fatwa za watu zinaweza kukosea au zikawa sahihi, ni mamoja awe mufti rasmi au asiye rasmi, awe mwalimu au asiye mwalimu. Fatwa zote zinapaswa kupimwa kwa Qur-aan na Sunnah. Kinacholingana navyo kinakubaliwa, na kinachowapinga kinakataliwa kutoka kwa yeyote aliyetamka maneno hayo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31706/هل-فتوى-المفتي-الرسمي-ملزمة-للناس
  • Imechapishwa: 09/03/2026