Hapa inakuwa ni wajibu kuacha wasia

Swali: Ni yepi maoni sahihi kuhusu wasia wa lazima? Ni nani miongoni mwa wanazuoni waliosema kuhusu wasia wa lazima?

Jibu: Wasia wa lazima ni kuhusu zile haki zilizo juu ya mtu. Inampasa aache wasia kuhusu madeni ambayo hana vielelezo navyo, kama vile kafara na haki za watu zilizo juu yake. Ni lazima aache wasia juu ya hayo. Kuhusu wasia wa sehemu ya urithi kama thuluthi, robo au khumusi ni aina ya wasia unaopendeza.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30985/ما-حكم-الوصية-ومتى-تكون-واجبة
  • Imechapishwa: 19/09/2025