Swali: Ni ipi hukumu ya makundi ya Kiislamu kushirikiana katika kupiga vita kanuni za watu zilizotungwa?

Jibu: Hili ni wajibu.

Swali: Ni ipi hukumu ya makundi ya Kiislamu kushirikiana katika kupiga vita kanuni za watu zilizotungwa? Kwa pamoja kikundi.

Swali: Ikiwa unakariri swali baada ya kukujibu ya kwamba ni wajibu, basi inaonekana una kitu kingine nyuma ya swali hili. Unamaanisha nini kwa neno “kushirikiana”?

Muulizaji: Kufanya uasi.

al-Albaaniy: Allaah akuongoze. Namna hii ndivyo mtu anavyouliza swali? Uasi unamaanisha maandamano haya.

Muulizaji: Ndio.

al-Albaaniy: Wewe inaonekana hukuwa katika siku za punde zilizoisha. Tulilizungumzia kwa kina jambo hili na kufikia ya kwamba maandamano haya ambayo yako kwa ajili ya kukemea baadhi ya kanuni ni njia za kigeni zisizojuzu kwa waislamu kuzifanya.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Juddah (32)
  • Imechapishwa: 28/01/2017