Hakuna katika ulimwengu mungu mwingine wa kuombwa zaidi ya Allaah

Swali: Ni ipi hukumu ya mtu kusema katika du´aa yake:

”Je, katika ulimwengu kuna mungu mwingine asiyekuwa Wewe aombwe?”

Jibu: Si katika ulimwengu, asiseme: ”Je.” Bali aseme: ”Hakuna katika ulimwengu” kwa njia ya kukanusha. Kuuliza kwa maana ya kusisitiza kwa nia hiyo. Kwa maana nyingine hakuna katika ulimwengu. Ama ikiwa ni kwa namna ya shaka, haijuzu.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31074/حكم-الدعاء-بـ-هل-في-الوجود-اله-سواك-فيدعى
  • Imechapishwa: 02/10/2025