192 – Muhammad bin Haatim bin Nu´aym ametukhabarisha: Hibbaan ametukhabarisha: ´Abdullaah ametukhabarisha, kutoka kwa Ma´mar, kutoka kwa Thumaamah bin ´Abdillaah bin Anas: Amemsikia Anas amesimulia kuhusu mjomba wake:

”Wakati Haraam bin Milhaan alipochomwa siku ya kisima cha Ma-uunah, alijipaka damu usoni na kichwani mwake na akasema: “Nimeshinda, naapa kwa Mola wa Ka’ba!”[1]

[1] al-Bukhaariy (4092) na Muslim (677).

  • Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 125
  • Imechapishwa: 29/09/2026