196 – Muhammad bin Haatim ametukhabarisha: Hibbaan ametukhabarisha: ´Abdullaah ametukhabarisha, kutoka kwa Muusa bin ´Aliy bin Rabaah: Nimemsikia baba yangu akisema: Nimemsikia ´Amr bin al-´Aasw akisema:

“Watu wa Madiynah waliingiwa na khofu pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), ndipo wakatawanyika. Nikamuona Saalim akiwa amekaa chini Msikitini huku mapaja yake yakiwa yamebana tumbo lake kwa mshipi wake wa upanga. Nilipoona hivyo, nikafanya vivyo hivyo. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akatoka na kuniona mimi na Saalim. Basi akawaendea watu na kusema: “Enyi watu! Ni kwa nini msitafute kinga kwa Allaah na Mtume Wake? Kwa nini hamkufanya kama walivofanya mabwana hawa wawili?”[1]

[1] Ahmad (4/203) na Ibn Hibbaan (7092), aliyeisahihisha.

  • Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 127
  • Imechapishwa: 29/09/2026