251 – Qutaybah bin Sa´iyd ametukhabarisha: Ghundar ametukhabarisha: Shu´bah ametukhabarisha, kutoka kwa ´Amr bin Murrah, kutoka kwa Murrah al-Hamadaaniy, kutoka kwa Abu Muusa, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:
”Wanaume wakamilifu ni wengi, lakini hawakukamilika katika wanawake isipokuwa Maryam bint ´Imraan na ´Aasiyah, mwanamke wa Fir´awn.”[1]
252 – Ibraahiym bin Ya´quub ametukhabarisha: Abun-Nu´maan ametukhabarisha: Daawuud bin Abiyl-Furaat ametuhadithia, kutoka kwa ´Ilbaa’ bin Ahmad, kutoka kwa ´Ikrimah, kutoka kwa Ibn ´Abbaas, ambaye ameeleza:
“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alichora mistari minne ardhini na akasema: “Je, mnajua ni nini?” Wakasema: ”Allaah na Mtume wake ndio wanajua zaidi.” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Wanawake bora kabisa wa Peponi ni Khadiyjah bint Khuwaylid, Faatwimah bint Muhammad, Maryam bint ´Imraan na Aasiyah bint Muzaahim, mwanamke wa Fir´awn.”[2]
[1] al-Bukhaariy (3411) na Muslim (2431).
[2] Ahmad (1/316). Swahiyh kwa mujibu wa Ahmad Shaakir katika “Musnad-ul-Imaam Ahmad” (3/279).
- Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 152
- Imechapishwa: 30/09/2026
251 – Qutaybah bin Sa´iyd ametukhabarisha: Ghundar ametukhabarisha: Shu´bah ametukhabarisha, kutoka kwa ´Amr bin Murrah, kutoka kwa Murrah al-Hamadaaniy, kutoka kwa Abu Muusa, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:
”Wanaume wakamilifu ni wengi, lakini hawakukamilika katika wanawake isipokuwa Maryam bint ´Imraan na ´Aasiyah, mwanamke wa Fir´awn.”[1]
252 – Ibraahiym bin Ya´quub ametukhabarisha: Abun-Nu´maan ametukhabarisha: Daawuud bin Abiyl-Furaat ametuhadithia, kutoka kwa ´Ilbaa’ bin Ahmad, kutoka kwa ´Ikrimah, kutoka kwa Ibn ´Abbaas, ambaye ameeleza:
“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alichora mistari minne ardhini na akasema: “Je, mnajua ni nini?” Wakasema: ”Allaah na Mtume wake ndio wanajua zaidi.” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Wanawake bora kabisa wa Peponi ni Khadiyjah bint Khuwaylid, Faatwimah bint Muhammad, Maryam bint ´Imraan na Aasiyah bint Muzaahim, mwanamke wa Fir´awn.”[2]
[1] al-Bukhaariy (3411) na Muslim (2431).
[2] Ahmad (1/316). Swahiyh kwa mujibu wa Ahmad Shaakir katika “Musnad-ul-Imaam Ahmad” (3/279).
Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 152
Imechapishwa: 30/09/2026
https://firqatunnajia.com/fadhilah-za-aasiyah-bint-muzaahim/