Sifa njema zote ni za Allaah, Mstahiki wa sifa na Mwenye kustahiki kuhimidiwa, himdi inayozidi kila himdi nyingine, kama ubora wa Allaah juu ya viumbe Wake. Ninashuhudia kwamba hapana anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah pekee, hali ya kuwa hana mshirika, na ninashuhudia kwamba Muhammad ni mja Wake na Mtume Wake, asiye na shaka katika ukweli wake. Allaah amsifu na ampe amani yeye, jamaa zake pamoja na Maswahabah wake, kwa muda wote ambao mawingu yanamimina mvua yake na radi yake inaponguruma.
Ama baada ya hayo;
Hiki ni kitabu katika Fiqh, nimekifupisha kadiri ya uwezo. Nimejitosheleza humo kwa mtazamo mmoja, ili kiwe tegemeo kwa msomaji wake, na ili asiichanganyikiwe haki kwa sababu ya tofauti za mitazamo na riwaya.
Baadhi ya ndugu zangu waliniomba nikifupishe ili kiwe karibu zaidi kwa walimu na kiwe rahisi kwa wanafunzi. Nikawakubalia ombi hilo, hali ya kumtegemea Allaah (Subhaanah) katika kutakasa nia kwa ajili ya uso Wake Mtukufu, na katika kupata msaada wa kufikia radhi Zake kuu. Naye ndiye Anayetutosheleza na Mbora wa kutegemewa. Nimeweka ndani yake Hadiyth Swahiyh kwa kutafuta baraka kupitia kwazo na kwa kuzitegemea. Nimezifanya kutoka katika vitabu vya Hadiyth Swahiyh ili nijitosheleze na kutonukuu vyanzo vyake kila mara.
- Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 11
- Imechapishwa: 30/09/2026
Sifa njema zote ni za Allaah, Mstahiki wa sifa na Mwenye kustahiki kuhimidiwa, himdi inayozidi kila himdi nyingine, kama ubora wa Allaah juu ya viumbe Wake. Ninashuhudia kwamba hapana anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah pekee, hali ya kuwa hana mshirika, na ninashuhudia kwamba Muhammad ni mja Wake na Mtume Wake, asiye na shaka katika ukweli wake. Allaah amsifu na ampe amani yeye, jamaa zake pamoja na Maswahabah wake, kwa muda wote ambao mawingu yanamimina mvua yake na radi yake inaponguruma.
Ama baada ya hayo;
Hiki ni kitabu katika Fiqh, nimekifupisha kadiri ya uwezo. Nimejitosheleza humo kwa mtazamo mmoja, ili kiwe tegemeo kwa msomaji wake, na ili asiichanganyikiwe haki kwa sababu ya tofauti za mitazamo na riwaya.
Baadhi ya ndugu zangu waliniomba nikifupishe ili kiwe karibu zaidi kwa walimu na kiwe rahisi kwa wanafunzi. Nikawakubalia ombi hilo, hali ya kumtegemea Allaah (Subhaanah) katika kutakasa nia kwa ajili ya uso Wake Mtukufu, na katika kupata msaada wa kufikia radhi Zake kuu. Naye ndiye Anayetutosheleza na Mbora wa kutegemewa. Nimeweka ndani yake Hadiyth Swahiyh kwa kutafuta baraka kupitia kwazo na kwa kuzitegemea. Nimezifanya kutoka katika vitabu vya Hadiyth Swahiyh ili nijitosheleze na kutonukuu vyanzo vyake kila mara.
Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 11
Imechapishwa: 30/09/2026
https://firqatunnajia.com/01-historia-ya-umdat-ul-fiqh-ya-ibn-qudaamah/