248 – ´Amr bin ´Aliy ametukhabarisha: Yahyaa ametukhabarisha: Shu´bah ametukhabarisha: ´Amr bin Murrah ametukhabarisha, kutoka kwa Murrah, kutoka kwa Abu Muusa, ambaye amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Wanaume wakamilifu ni wengi, lakini hawakukamilika katika wanawake isipokuwa Maryam bint ´Imraan na ´Aasiyah, mwanamke wa Fir´awn.”[1]

249 – Ahmad bin Harb ametukhabarisha: Mu´aawiyah ametukhabarisha, kutoka kwa Hishaam, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa ´Abdullaah bin Ja´far, kutoka kwa ´Aliy, ambaye ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mwanamke wao mbora ni Maryam bint ´Imraan na mwanamke wao mbora ni Khadiyjah.”[2]

250 – al-´Abbaas bin Muhammad ametukhabarisha: Yuunus ametukhabarisha: Daawuud bin Abiyl-Furaat ametuhadithia, kutoka kwa ´Aliy, kutoka kwa ´Ikrimah, kutoka kwa Ibn ´Abbaas, ambaye ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Wanawake bora wa Peponi ni Khadiyjah bint Khuwaylid, Faatwimah bint Muhammad, Maryam bint ´Imraan na Aasiyah bint Muzaahim, mwanamke wa Fir´awn.”[3]

[1] al-Bukhaariy (3411) na Muslim (2431).

[2] al-Bukhaariy (3815) na Muslim (2430).

[3] Ahmad (1/316). Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh kwa mujibu wa Ahmad Shaakir katika “Musnad-ul-Imaam Ahmad” (3/279).

  • Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 150-151
  • Imechapishwa: 30/09/2026