Swali: Mwanamke amemfisha mume wake miaka mitano iliyopita. Ana watoto wawili wasioswali. Mkubwa ana miaka 19 na mwingine ana miaka 17. Nimewaamrisha kuswali, nikawanasihi na kuwaeleza ukhatari wa kuacha swalah lakini haikufua dafu. Jengine ni kwamba ni mgonjwa na kila akiwaona katika hali hiyo anaathirika, ambapo wanaanza kuswali kisha baadaye wanaacha. Awafanye nini? Je, anapata dhambi akiwaacha?
Jibu: Hapana shaka kwamba dhambi wanapata watoto, kwa sababu wameshabaleghe. Kuacha swalah ni kufuru inayomtoa mtu katika Uislamu. Hilo ni kwa dalili nyingi ndani ya Qur-aan na Sunnah. Baadhi ya wanazuoni wamesimulia maafikiano ya Maswahabah juu ya hilo. Hapana shaka kwamba ambaye haswali hakuna moyoni mwake imani. Kwa sababu imani inapelekea matendo, na utiifu mkubwa wa kimwili ni swalah. Kwa hiyo akiacha kuswali ni dalili ya kwamba moyoni mwake hakuna imani ingawa atadai kuwa ni muumini. Imani inapelekea kutoka kwa muumini kuhakikisha utiifu huu mtukufu.
Kuhusu wewe, ni lazima kwako kumcha Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) katika kuwanasihi, kuwaelekeza, kuwaamrisha kuswali, kuwakataza kuipoteza, kuwaamsha kutoka usingizini na kuwagombeza kuitekeleza. Pamoja na hayo yote wasiposwali, hesabu yao iko kwa Allaah (´Azza wa Jall). Waombee du´aa kwa wingi ya kuongozwa na kuwafikishwa. Pengine Allaah akakuitikia na hivyo ikawa ndio furaha na kufaulu kwako wewe na wao hadi siku ya Qiyaamah.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/38-39)
- Imechapishwa: 25/03/2026
Swali: Mwanamke amemfisha mume wake miaka mitano iliyopita. Ana watoto wawili wasioswali. Mkubwa ana miaka 19 na mwingine ana miaka 17. Nimewaamrisha kuswali, nikawanasihi na kuwaeleza ukhatari wa kuacha swalah lakini haikufua dafu. Jengine ni kwamba ni mgonjwa na kila akiwaona katika hali hiyo anaathirika, ambapo wanaanza kuswali kisha baadaye wanaacha. Awafanye nini? Je, anapata dhambi akiwaacha?
Jibu: Hapana shaka kwamba dhambi wanapata watoto, kwa sababu wameshabaleghe. Kuacha swalah ni kufuru inayomtoa mtu katika Uislamu. Hilo ni kwa dalili nyingi ndani ya Qur-aan na Sunnah. Baadhi ya wanazuoni wamesimulia maafikiano ya Maswahabah juu ya hilo. Hapana shaka kwamba ambaye haswali hakuna moyoni mwake imani. Kwa sababu imani inapelekea matendo, na utiifu mkubwa wa kimwili ni swalah. Kwa hiyo akiacha kuswali ni dalili ya kwamba moyoni mwake hakuna imani ingawa atadai kuwa ni muumini. Imani inapelekea kutoka kwa muumini kuhakikisha utiifu huu mtukufu.
Kuhusu wewe, ni lazima kwako kumcha Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) katika kuwanasihi, kuwaelekeza, kuwaamrisha kuswali, kuwakataza kuipoteza, kuwaamsha kutoka usingizini na kuwagombeza kuitekeleza. Pamoja na hayo yote wasiposwali, hesabu yao iko kwa Allaah (´Azza wa Jall). Waombee du´aa kwa wingi ya kuongozwa na kuwafikishwa. Pengine Allaah akakuitikia na hivyo ikawa ndio furaha na kufaulu kwako wewe na wao hadi siku ya Qiyaamah.
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/38-39)
Imechapishwa: 25/03/2026
https://firqatunnajia.com/endelea-kuwanasihi/