Swali: Je, inajuzu kuomba kwenye Sujuud kwa du´aa za Qur-aan? Kwa mfano maneno:

قَالَا رَبَّنَا ظَلَمْنَا أَنفُسَنَا وَإِن لَّمْ تَغْفِرْ لَنَا وَتَرْحَمْنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ

“Wakasema: “Mola wetu! Tumedhulumu nafsi zetu na basi usipotusamehe na ukaturehemu, basi bila shaka tutakuwa miongoni mwa waliokhasirika.” (07:23)

na Aayah nyinginezo ambazo ziko na du´aa kutoka kwenye Qur-aan?

Jibu: Ni sawa kufanya hivo kwa kuwa makusudio yako sio kusoma Qur-aan. Bali makusudio yako ni kuomba du´aa. Haina neo kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (23) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1428-3-14.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020