Swali: Tunapomzika maiti, ni maneno gani sahihi tunayopaswa kusema kwa kufuata amri ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Muombeni msamaha ndugu yenu na muombeeni athibitishe, kwani hakika hivi sasa anahojiwa.”?
Jibu: Wakati wa kumzika husemwa:
بسم الله وعلى ملة رسول الله
“Tunaanza kwa jina la Allaah na juu ya Sunnah ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”
Baada ya kumaliza kumzika, inapendekezwa wasimame karibu naye na waseme:
“Ee Allaah! Msamehe fulani! Ee Allaah! Msameh! Ee Allaah! Mthibitishe kwa kauli thabiti.”
Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akimaliza mazishi, husimama juu ya maiti na kusema:
“Ee Allaah msamehe na mthibitishe kwa kauli thabiti!”
Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Muombeni msamaha ndugu yenu na muombeeni athibitishe, kwani hakika hivi sasa anahojiwa.”
Hivyo anaombewa msamaha, rehema na uthabiti juu ya haki. Wanasimama kwa muda mfupi kisha wanaondoka.
Swali: Je, waelekee Qiblah?
Jibu: Si lazima, hapana, si lazima, kwa hali yoyote ile.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3250/الذكر-الوارد-عند-دفن-الميت-وبعد-الفراغ-من-دفنه
- Imechapishwa: 10/10/2026
Swali: Tunapomzika maiti, ni maneno gani sahihi tunayopaswa kusema kwa kufuata amri ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Muombeni msamaha ndugu yenu na muombeeni athibitishe, kwani hakika hivi sasa anahojiwa.”?
Jibu: Wakati wa kumzika husemwa:
بسم الله وعلى ملة رسول الله
“Tunaanza kwa jina la Allaah na juu ya Sunnah ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”
Baada ya kumaliza kumzika, inapendekezwa wasimame karibu naye na waseme:
“Ee Allaah! Msamehe fulani! Ee Allaah! Msameh! Ee Allaah! Mthibitishe kwa kauli thabiti.”
Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akimaliza mazishi, husimama juu ya maiti na kusema:
“Ee Allaah msamehe na mthibitishe kwa kauli thabiti!”
Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Muombeni msamaha ndugu yenu na muombeeni athibitishe, kwani hakika hivi sasa anahojiwa.”
Hivyo anaombewa msamaha, rehema na uthabiti juu ya haki. Wanasimama kwa muda mfupi kisha wanaondoka.
Swali: Je, waelekee Qiblah?
Jibu: Si lazima, hapana, si lazima, kwa hali yoyote ile.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3250/الذكر-الوارد-عند-دفن-الميت-وبعد-الفراغ-من-دفنه
Imechapishwa: 10/10/2026
https://firqatunnajia.com/duaa-wakati-wa-kumzika-na-kumaliza-kumzika-maiti/