al-Waziyr bin al-Hinzaabah amesema: Nilimsikia Muhammad bin Muusa al-Ma´muuniy – swahiba wa an-Nasaa´iy – akisema:
“Niliwasikia baadhi ya watu namna wakimkaripia Abu ´Abdir-Rahmaan an-Nasaa´iy kwa ajili ya kuandika kitabu kinachozungumzia fadhilah za ´Aliy na kuacha kuandika fadhilah za Abu Bakr na ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhum). Nikazungumza naye suala hilo ambapo akasema: “Nilipofika Dameski nilikuta watu wana ufahamu wa kimakosa juu ya ´Aliy ndio maana nikawa nimeandika kitabu “al-Khaswaa-isw” kwa kutaraji Allaah (Ta´ala) atawaongoza.” Kisha baada ya hapo akaandika “Fadhwaa-il-us-Swahaabah”. Nikasikia akiambiwa na mimi huku nasikia: “Unasemaje juu ya kuandika kitabu juu ya fadhilah za Mu´aawiyah (Radhiya Allaahu ´anh)?” Akasema: “Niandike nini?” Hadiyth:
“Ee Allaah! Usilishibishe tumbo lake!”[1]
Muulizaji akakaa kimya.”
Pengine mtu anaweza kusema kuwa hii ni sifa nzuri kwa Mu´aawiyah, kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Ee Allaah! Ambaye nimemlaani au kumtukana basi nakuomba ujaalie hayo kwake iwe ni utakaso na rehema.”[2]
[1] Muslim (2604) na Abu Daawuud at-Twayaalisiy (2688).
[2] Muslim (2600).
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (14/129-130)
- Imechapishwa: 12/11/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)