Swali: Ni lini mtu atasema:
اللّهُـمَّ إِنِّـي ظَلَـمْتُ نَفْسـي ظُلْمـاً كَثـيراً وَلا يَغْـفِرُ الذُّنـوبَ إِلاّ أَنْت، فَاغْـفِر لي مَغْـفِرَةً مِنْ عِنْـدِك وَارْحَمْـني إِنَّكَ أَنْتَ الغَـفورُ الرَّحـيم
”Ee Allaah! Hakika mimi nimeidhulumu nafsi yangu dhuluma nyingi na hakuna asamehaye dhambi isipokuwa Wewe. Hivyo basi, nisamehe msamaha kutoka Kwako na unirehemu. Kwani hakika Wewe ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”[1]?
Jibu: Hili husemwa mwishoni mwa swalah kabla hajatoa salamu. Ni sawa pia akisema baada ya salamu na baada ya kuleta Dhikr. Hata hivyo kuomba kabla ya salamu ni bora na kamilifu zaidi, kwa sababu huo ndio wakati wa du´aa. Aombe kwa du´aa hii wakati wowote, kwani imepokelewa katika Hadiyth ya as-Swiddiyq kwamba aliiomba ndani ya swalah yake na ndani ya nyumba yake, kama alivyopokea Muslim pia. Kwa hiyo aiombe ndani ya swalah yake, katika nyumba yake, njiani au mahali popote. Ni du´aa kubwa. Ni du´aa kubwa ambayo inafaa kuombwa ndani ya swalah, katika sujuud, mwishoni mwa Tashahhud na katika wakati wowote.
[1] al-Bukhaariy (6326) na Muslim (2705).
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31204/متى-يقال-اللهم-اني-ظلمت-نفسي-ظلما-كثيرا
- Imechapishwa: 13/10/2025
Swali: Ni lini mtu atasema:
اللّهُـمَّ إِنِّـي ظَلَـمْتُ نَفْسـي ظُلْمـاً كَثـيراً وَلا يَغْـفِرُ الذُّنـوبَ إِلاّ أَنْت، فَاغْـفِر لي مَغْـفِرَةً مِنْ عِنْـدِك وَارْحَمْـني إِنَّكَ أَنْتَ الغَـفورُ الرَّحـيم
”Ee Allaah! Hakika mimi nimeidhulumu nafsi yangu dhuluma nyingi na hakuna asamehaye dhambi isipokuwa Wewe. Hivyo basi, nisamehe msamaha kutoka Kwako na unirehemu. Kwani hakika Wewe ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”[1]?
Jibu: Hili husemwa mwishoni mwa swalah kabla hajatoa salamu. Ni sawa pia akisema baada ya salamu na baada ya kuleta Dhikr. Hata hivyo kuomba kabla ya salamu ni bora na kamilifu zaidi, kwa sababu huo ndio wakati wa du´aa. Aombe kwa du´aa hii wakati wowote, kwani imepokelewa katika Hadiyth ya as-Swiddiyq kwamba aliiomba ndani ya swalah yake na ndani ya nyumba yake, kama alivyopokea Muslim pia. Kwa hiyo aiombe ndani ya swalah yake, katika nyumba yake, njiani au mahali popote. Ni du´aa kubwa. Ni du´aa kubwa ambayo inafaa kuombwa ndani ya swalah, katika sujuud, mwishoni mwa Tashahhud na katika wakati wowote.
[1] al-Bukhaariy (6326) na Muslim (2705).
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31204/متى-يقال-اللهم-اني-ظلمت-نفسي-ظلما-كثيرا
Imechapishwa: 13/10/2025
https://firqatunnajia.com/duaa-ambayo-abu-bakr-alikuwa-akiomba-mwishoni-mwa-tashahhud/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket