Swali: Je, subira ina daraja moja tu au ina daraja nyingi?

Jibu: Ina daraja tatu zilizobainishwa:

1 – Subira juu ya misiba kwa moyo wake.

2 – Kwa ulimi wake.

3 – Kwa viungo vyote.

Daraja tatu; kwa moyo, kwa maana kwamba asisononeke wala kukata tamaa, kwa ulimi, kwa maana kwamba asiseme yasiyofaa kama kuomboleza, matusi na maneno machafu, na kwa viungo, kwa maana kwamba asijipige uso, asirarue nguo, asijipige shavuni na wala kujimwagia vumbi au mfano wa hayo.

Swali: Mtu akishukuru kwa ulimi wake lakini akafanya kinyume kwa viungo vyake?

Jibu: Huyo hatakuwa mwenye subira.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31125/ما-مراتب-الصبر-وهل-يكفي-باللسان
  • Imechapishwa: 04/10/2025