Damu ya uzazi imekatika kisha ikamrudia mara nyingine

Swali: Mwanamke alikua ananyonyesha, akaingia mwezi wa Ramadhaan akiwa katika hali ya damu ya uzazi. Baada ya siku 27 alipojifungua alitoka katika hali ya nifasi akajitwahirisha kisha akaanza kufunga. Kabla ya kumalizika kwa mwezi wa Ramadhaan kwa siku saba, akapata tena damu na akaendelea nayo kwa siku sita. Je, hiyo damu inazingatiwa kama damu ya uzazi au ni damu ya hedhi? Kwa sababu kawaida yake ya hedhi inadumu siku sita.

Jibu: Mwanamke aliyejifungua hana kizuizi cha kuoga ikiwa amejisafisha. Ni lazima kwake kuoga pindi atakapojitwahirisha, hata kama amebaki na siku kumi au ishirini. Hakuna kipindi maalum cha chini cha nifasi, kwani inaweza kuwa ya muda mfupi au mrefu. Hivyo ikiwa amesafiika kwa siku kumi, ishirini, hata ishirini na tano au ishirini na saba, basi ni lazima aoge, aswali, afunge na kuwa halali kwa mume wake. Ikiwa damu itarudi ndani ya kipindi cha siku arobaini za nifasi, basi atapaswa kukaa kando na asiswali wala kufunga, kwani hiyo itakuwa ni damu ya uzazi mpaka akamilishe muda wa nifasi wa  siku arobaini. Ikiwa atakamilisha siku arobaini, atapaswa kuoga na kuendelea na ´ibaadah zake na atakuwa halali kwa mume wake, kwa kuwa mwisho wa nifasi ni siku arobaini, kama ilivyotajwa katika Hadiyth ya Umm Salamah. Damu inayokuja baada ya hii itachukuliwa kuwa ni damu ya ugonjwa ambayo haimzuii swalah, kufunga wala ushirikiano na mume. Atapaswa kufanya kama alivyofanya mwanamke mwenye dam ya ugonjwa. Kwa maana kwamba ataswali baada ya kuingia kwa wakati wa swalah, atajisafisha kwa maji na kutawadha juu ya kila swalah. Anaweza pia kuunganisha swalah mbili, kwa sababu yuko katika hali inayoshabihiana na ugonjwa. Lakini hatoswali isipokuwa kwa wudhuu´ mpya. Kila wakati wa swalah,  atajisafisha, atafanya wudhuu´ na kuswali kama inavyohitajika. Vilevile anaweza kukusanya baina ya swalah Dhuhr na ´Aswr, Maghrib na Isha, kama ilivyopokelewa kutoka kwa Ramlah bint Jahsh (Radhiya Allaahu ‘anhaa).

Kwa kifupi ni kwamba ni sawa ikiwa amesafisha katikati ya siku arobaini. Baada ya hapo atapaswa kuoga, kuswali, afunge na kuwa halali kwa mume wake. Ikiwa damu itarudi ndani ya siku arobaini, hatoswali na kufunga ndani ya siku arobaini hizi. Hiyo damu iliyorudi sio hedhi, bali ni damu ya ugonjwa muda wa kuwa ni ndani ya siku arobaini. Kisha akisafika kabla ya arobaini, ataoga na kuswali. Damu ikizidi baada ya siku arobaini, ataoga na kuswali. Haijalishi kitu hata kama damu bado inamtoka. Kwa sababu damu ya uzazi haizidi siku arobaini kwa mujibu wa maoni sahihi. Kwa hiyo ataoga, ataswali na kufunga hata kama bado anatokwa na damu. Hata hivyo asitawadhe isipokuwa baada ya kuingia wakati wa kila swalah. Kwa maana wakati wa swalah ukiingia ndio atatawadha, atajisafisha kwa maji, atatawadha juu ya wakati wa kila swalah. Namna hii ndio imepokelewa juu ya nwanamke mwenye damu ya ugonjwa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3375/حكم-انقطاع-دم-النفاس-ثم-ظهوره-مرة-اخرى
  • Imechapishwa: 22/09/2026