Swali: Swali hili linawahusu madaktari. Wanaona kwamba huenda wakahitajia katika upasuaji saa nyingi zaidi, zikapita ndani yake nyakati kadhaa za swalah. Kukatisha upasuaji ili kuswali kuna khatari kwa mgonjwa. Ni vipi unakuwa wakati wao kwa nisba ya swalah?
Jibu: Huu ni udhuru unaokubalika katika Shari´ah. Ni kama vile wapiganaji vita huenda wakalazimika kuchelewesha swalah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) siku ya Ahzaab alilazimika mpaka akaswali ´Aswr baada ya Maghrib kwa sababu ya vita. Maswahabah kule Tustar nchini ´Iraaq katika vita dhidi ya wafursi, kulipokucha hawakuweza kuswali swalah ya Fajr, kwa kuwa walikuwa kwenye malango ya mji, baadhi yao juu ya kuta na baadhi tayari wameingia mjini. Matokeo yake wakaichelewesha mpaka wakati wa mchana. Hivyo basi ikiwa mpo katika upasuaji na mkiacha kuna khatari kwa mgonjwa; endeleeni nao japo muda wa swalah utapita, kisha swalini baada ya hapo. Wala hakuna tatizo na himdi zote ni za Allaah. Hivi ndio usawa.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30055/حكم-تاخير-الصلاة-لاجراء-العمليات-الجراحية
- Imechapishwa: 05/09/2025
Swali: Swali hili linawahusu madaktari. Wanaona kwamba huenda wakahitajia katika upasuaji saa nyingi zaidi, zikapita ndani yake nyakati kadhaa za swalah. Kukatisha upasuaji ili kuswali kuna khatari kwa mgonjwa. Ni vipi unakuwa wakati wao kwa nisba ya swalah?
Jibu: Huu ni udhuru unaokubalika katika Shari´ah. Ni kama vile wapiganaji vita huenda wakalazimika kuchelewesha swalah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) siku ya Ahzaab alilazimika mpaka akaswali ´Aswr baada ya Maghrib kwa sababu ya vita. Maswahabah kule Tustar nchini ´Iraaq katika vita dhidi ya wafursi, kulipokucha hawakuweza kuswali swalah ya Fajr, kwa kuwa walikuwa kwenye malango ya mji, baadhi yao juu ya kuta na baadhi tayari wameingia mjini. Matokeo yake wakaichelewesha mpaka wakati wa mchana. Hivyo basi ikiwa mpo katika upasuaji na mkiacha kuna khatari kwa mgonjwa; endeleeni nao japo muda wa swalah utapita, kisha swalini baada ya hapo. Wala hakuna tatizo na himdi zote ni za Allaah. Hivi ndio usawa.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30055/حكم-تاخير-الصلاة-لاجراء-العمليات-الجراحية
Imechapishwa: 05/09/2025
https://firqatunnajia.com/daktari-kuchelewesha-swalah-kwa-sababu-ya-upasuaji-wa-masaa-mengi/