Chenye kuzidi juu ya dufu

Swali: Je, inajuzu kucheza na kuimba usiku wa harusi na kupiga dufu, ngoma na makofi?

Jibu: Sunnah ni kupiga dufu kwa ajili ya kutangaza ndoa. Hilo linafanywa na wanawake peke yao. Kinachozidi juu ya dufu ni miongoni mwa mambo yasiyostahiki kwa mwanamke wa kiislamu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Tangazeni ndoa hii na ipigieni dufu.”

Huku ni kutangaza na kuonyesha ndoa. Kinachozidi juu ya dufu ni mambo ambayo ima yakawa yenye kuchukiza au pengine yakawa ya haramu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/حكم-الرقص-والغناء-في-ليلة-الزفاف
  • Imechapishwa: 12/06/2022