Mtu akishachinja ale kile kiasi anachotaka. Asitosheke na kipande kidogo. Bali ale anachotaka. Akichinja kichinjwa ale yeye na familia yake kiasi kikubwa au kidogo. Sunnah ni yeye kula, alishe chakula kwa kiasi anachoweza na atoe swadaqah na zawadi kutoka katika kichinjwa hichi kwa kiasi anachoweza. Bora amgawe mara tatu:

1 – Theluthi moja wale wao.

2 – Theluthi nyingine waitoe kwa jamaa na marafiki zao.

3 – Theluthi nyingine wawape mafukara.

Hapana vibaya pia wakila sehemu yake kubwa na wakatoa swadaqah sehemu yake ndogo. Jambo ni lenye wasaa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewaamrisha wale na walisha chakula. Allaah amesema:

فَكُلُوا مِنْهَا وَأَطْعِمُوا الْبَائِسَ الْفَقِيرَ

“Basi kuleni humo na lisheni ambaye ni fakiri mno.”[1]

Kwa hivyo anatakiwa kuwapa masikini kile kiasi kitachowezekana katika mnyama huo. Bora ni yeye kuwapa mafukara theluthi. Ni vyema pia akiwapa theluthi nyingine jamaa zake na majirani zake. Udhhiyah inasihi endapo asitoe zawadi au akatoa swadaqah kiasi kidogo au asitoe kabisa. Udhhiyah yake inasihi na inakubalika kwa mujibu wa Shari´ah. Hata hivyo baadhi ya wanazuoni wameona kuwa ni wajibu wake kutoa nyama kidogo ili kufanyia kazi maneno Yake (Ta´ala):

فَكُلُوا مِنْهَا وَأَطْعِمُوا الْبَائِسَ الْفَقِيرَ

“Basi kuleni humo na lisheni ambaye ni fakiri mno.”

Atoe kile kiasi cha nyama anachoweza hata kama sio ile Udhhiyah ikiwa ameshaila. Atoe nyama nyingine ili awe ametekeleza wajibu huu. Kwa hali yoyote Sunnah ni yeye kutoa sehemu yake:

فَكُلُوا مِنْهَا وَأَطْعِمُوا الْبَائِسَ الْفَقِيرَ

“Basi kuleni humo na lisheni ambaye ni fakiri mno.”

فَكُلُوا مِنْهَا وَأَطْعِمُوا الْقَانِعَ وَالْمُعْتَرَّ

“Kuleni kutoka humo na lisheni waliokinai.”[2]

Hivo ndivo alivosema Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kuleni, toeni swadaqah na wekeni akiba.”

[1] 22:28

[2] 22:36

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/17196/حكم-الاضحية-في-عيد-الاضحى-وكيفيتها
  • Imechapishwa: 14/06/2024