Swali: Ninaposwali kwenye msikiti Haram hufunika uso wangu kwa sababu kuna wanaume wasiokuwa Mahram karibu nami. Lakini ninaposujudu huondoa kifuniko hicho ili uso wangu uguse ardhi wakati wa kusujudu. Ni ipi hukumu ya kitendo changu hiki?

Jibu: Kitendo hiki ni kizuri, kwa sababu mwenye kuswali kuugusa uso wake moja kwa moja ardhini ni bora zaidi. Hata hivyo akisujudu juu ya mtandio wake pia hakuna ubaya.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/291)
  • Imechapishwa: 06/03/2026