Swali: Baadhi ya wale wanaouza mbwa waliofunzwa wanajengea hoja kwamba wanawauza kwa ajili ya ule muda waliotumia na kuwafanyia bidii na si kuuzwa mbwa yeye kama yeye. Je, haya ni sahihi?

Jibu: Hii ni njia moja wapo ya hila. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza chumo la mbwa na wewe unataka kulifanyia hilo njama  na unasema kuwa eti unamuuza kwa mkabala wa ule uangalizi uliofanya. Haijuzu kufanya biashara ya mbwa hata kama watakuwa wamepewa mafunzo. Lakini kinachofaa ni kule kuwatumia peke yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (27)
  • Imechapishwa: 18/04/2021