Swali: Kutoka kwa ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz kwenda kwa ndugu mtukufu X – Allaah amjaalie tawfiyq katika kila kheri na amzidishie elimu na imani. Aamiyn.
Swali lenu linahusu kusoma Basmalah kwa sauti ya juu na kutoitikia ”Aamiyn”?
Jibu: Bora ni kusema Basmalah kimyakimya. Hilo ni kutokana na maneno Anas (Radhiya Allaahu ´anh):
”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Abu Bakr na ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) hawakuwa wakisoma “Bismillaahi ar-Rahmaan ar-Rahiym” kwa sauti ya juu. Ikiwa mtu atasoma kwa sauti ya juu katika baadhi ya nyakati kwa lengo la kufundisha, basi hakuna ubaya. Kwa sababu imethibiti kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) kinachofahamisha hivo.
Kuhusu kuitikia ”Aamiyn”, Sunnah ni kuileta baada ya neno:
وَلاَ الضَّالِّينَ
”… na wala wale waliopotea!”
katika swalah na nje ya swalah. Kwa sababu imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba alikuwa akifanya hivyo na akasema:
“Imamu anaposema:
وَلاَ الضَّالِّينَ
”… na wala wale waliopotea!”
basi semeni:
”Aamiyn.”
kwani yule ambaye Aamiyn yake itaenda sambamba na Aamiyn ya Malaika, basi atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia.”
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/247)
- Imechapishwa: 04/03/2026
Swali: Kutoka kwa ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz kwenda kwa ndugu mtukufu X – Allaah amjaalie tawfiyq katika kila kheri na amzidishie elimu na imani. Aamiyn.
Swali lenu linahusu kusoma Basmalah kwa sauti ya juu na kutoitikia ”Aamiyn”?
Jibu: Bora ni kusema Basmalah kimyakimya. Hilo ni kutokana na maneno Anas (Radhiya Allaahu ´anh):
”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Abu Bakr na ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) hawakuwa wakisoma “Bismillaahi ar-Rahmaan ar-Rahiym” kwa sauti ya juu. Ikiwa mtu atasoma kwa sauti ya juu katika baadhi ya nyakati kwa lengo la kufundisha, basi hakuna ubaya. Kwa sababu imethibiti kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) kinachofahamisha hivo.
Kuhusu kuitikia ”Aamiyn”, Sunnah ni kuileta baada ya neno:
وَلاَ الضَّالِّينَ
”… na wala wale waliopotea!”
katika swalah na nje ya swalah. Kwa sababu imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba alikuwa akifanya hivyo na akasema:
“Imamu anaposema:
وَلاَ الضَّالِّينَ
”… na wala wale waliopotea!”
basi semeni:
”Aamiyn.”
kwani yule ambaye Aamiyn yake itaenda sambamba na Aamiyn ya Malaika, basi atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia.”
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/247)
Imechapishwa: 04/03/2026
https://firqatunnajia.com/basmalah-inasemwa-kimyakimya-aamiyn-kwa-sauti-ya-juu/