Swali: Ni ipi hukumu ya mtu anayesikia nyimbo na kuandika maneno ya nyimbo, kwa maana yeye ni mshairi na anawapa waimbaji maneno yake ili waimbe? Ni ipi hukumu ya kuandika mashairi hayo na kuwapa wasanii wayaimbe?
Jibu: Anapata dhambi na ni msaidizi katika dhambi. Ni mwenye dhambi na msaidizi katika dhambi. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:
وَمِنَ النَّاسِ مَن يَشْتَرِي لَهْوَ الْحَدِيثِ لِيُضِلَّ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ بِغَيْرِ عِلْمٍ وَيَتَّخِذَهَا هُزُوًا ۚ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ مُّهِينٌ وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِ آيَاتُنَا وَلَّىٰ مُسْتَكْبِرًا كَأَن لَّمْ يَسْمَعْهَا كَأَنَّ فِي أُذُنَيْهِ وَقْرًا ۖ فَبَشِّرْهُ بِعَذَابٍ أَلِيمٍ
”Miongoni mwa watu yuko ambaye ananunua maneno ya upuuzi ili awapoteze watu na Njia ya Allaah bila elimu na huzichukulia [Aayah Zake] mzaha. Hao watapata adhabu ya kutweza. Na anaposomewa Aayah Zetu, basi hugeuka huku akifanya kiburi kana kwamba hazisikii, kana kwamba kuna uziwi masikioni mwake. Basi mbashirie adhabu iumizayo.”[1]
Maneno ya upuuzi ni nyimbo kwa mujibu wa kikosi kikubwa cha wanazuoni, kwa wanazuoni wengi. Maana ya “ananunua” ni kwamba anachukua badala; anaweza kuyachukua bila ya thamani au kwa thamani, anaweza kununua nyimbo kwa thamani au kuyachukua bila ya thamani. Anafanya hivo ili apoteze na Njia ya Allaah. Kuna visomo viwili (لِيُضِلَّ) na (لِيَضِلَّ); ili apoteze kwa sababu ya matendo yake, na ili yeye apotee kwa sababu ya kujihusisha kwake na jambo hili la uovu bila ya elimu, anampoteza mwingine na anajipoteza yeye mwenyewe bila ya kuhisi yaliyo mpata katika balaa. Watu wengi wanaweza kudhani kwamba wako sahihi au kudhani hawana kosa lolote, hali ya kuwa wamepotea na wanapoteza na hawajui.
Kisha balaa hii ya kusikia nyimbo na kuburudika nazo, humpelekea baadaye kwenda kwenye kuzibeza Aayah za Allaah na kujikweza kuzisikia. Yule aliyezoea nyimbo na kuzipenda, basi inakuwa nzito kwake kusikia Qur-aan na kufurahia Qur-aan. Huenda akaibeza pia, akajikweza kusikia na kufanyia kazi, kwa sababu hiyo imekuja kutoka kwa ´Abdullaah bin Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) – naye ni miongoni mwa Maswahabah wakubwa na wanazuoni wao – alikuwa anaapa juu ya Aayah hii na anasema:
”Naapa kwa Allaah! Hakika nyimbo ni maneno ya upuuzi.”
Amesema tena:
”Hakika huotesha unafiki katika moyo kama maji yanavyootesha mmea.”
Maana yake ni nini? Maana yake akizoea nyimbo, basi inakuwa nzito kwake kusikia kheri na kupenda kheri na kukaa na watu wa kheri, basi unafiki unamea katika moyo wake. Kwa sababu unafiki ni kuchukia kheri, kupenda shari na kujionyesha kwa kheri huku yeye si katika watu wa kheri. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:
إِنَّ الْمُنَافِقِينَ يُخَادِعُونَ اللَّـهَ وَهُوَ خَادِعُهُمْ وَإِذَا قَامُوا إِلَى الصَّلَاةِ قَامُوا كُسَالَىٰ يُرَاءُونَ النَّاسَ وَلَا يَذْكُرُونَ اللَّـهَ إِلَّا قَلِيلًا
“Hakika wanafiki wanafikiri wanamhadaa Allaah na hali Yeye ndiye Mwenye kuwahadaa na wanaposimama kuswali basi husimama kwa uvivu, wakijionyesha kwa watu na wala hawamtaji Allaah isipokuwa kidogo tu.”[2]
Haya ni katika sifa zao: uvivu na uzito katika swalah na wanajionyesha kuwa wao ni waislamu na ni watu wema, lakini si hivyo. Katika sifa zao ni kughafilika na uchache wa kumtaja Allaah. Hivyo balaa hii ya nyimbo, kuburudika na nyimbo, kujihusisha nazo, kuzitumia na kuziuza na kuzinunua ni miongoni mwa sababu za maradhi ya nyoyo, kupendezesha batili, kuifanya iwe nzito kheri na kuielekeza nafsi katika upuuzi na mizaha badala ya kusikia Aayah za Allaah. Kisha inaweza kupelekea katika kupotea yeye mweyewe, kupoteza wengine, kubeza Qur-aan, kujikweza kusikia, kuisoma na mfano wa hayo. Kwa hiyo anaposikia Qur-aan hugeuka na anaposikia Qur-aan ya shaytwaan huja.
Swali: Hilo hata kama ni nyimbo zisizo na muziki?
Jibu: Hata kama hazina muziki, lakini kama zina muziki, basi shari inakuwa kubwa zaidi na dhambi inakuwa kubwa zaidi. Ikiwa zimembatana na ala kama rababa, muziki na kinamda, basi dhambi inakuwa kubwa zaidi.
[1] 31:06-07
[2] 04:142
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3412/حكم-استماع-الاغاني-وكتابة-اشعارها
- Imechapishwa: 09/09/2026

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3412/حكم-استماع-الاغاني-وكتابة-اشعارها
Imechapishwa: 09/09/2026
https://firqatunnajia.com/baadhi-ya-madhara-ya-muziki-na-nyimbo/