Swali: Ikiwa mtu amefanya Adhkaar kisha akaona katika ndoto yake kitu kinachomsikitisha – je, kinakuwa na athari yoyote?

Jibu: Afanye kama alivyoelekeza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)[1]. Akiona ndoto inayomsikitisha, basi afanye kama alivyofundisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), achukue adabu za Kishari´ah. Kabla ya kulala aseme:

بِاسْـمِكَ اللّهُـمَّ أَمـوتُ وَأَحْـيا

”Kwa jina lako, ee Allaah, ninakufa na ninakuwa hai.”

بِاسْمِكَ رَبِّـي وَضَعْـتُ جَنْـبي، وَبِكَ أَرْفَعُـه، فَإِن أَمْسَـكْتَ نَفْسـي فَاغْفِرْ لَهَا، وَإِنْ أَرْسَلْتَـها فاحْفَظْـها بِمـا تَحْفَـظُ بِه عِبـادَكَ الصّـالِحـين

”Kwa jina lako, Mola wangu, nimeweka ubavu wangu na kwa ajili Yako nitaunyanyua. Ukiizuia roho yangu, basi isamehe, na ukiirejesha, basi ihifadhi kwa yale unachowahifadhi kwayo waja Wako wema.”[2]

Kisha asome Aayatul-Kursiy na al-Ikhlaasw, al-Falaq na an-Naas mara tatu. Haya yote ni katika Sunnah na kinga za Kishari´ah.

Vilevile aseme mwishoni mwa du´aa zake:

اللّهُـمَّ أَسْـلَمْتُ نَفْـسي إِلَـيْكَ، وَفَوَّضْـتُ أَمْـري إِلَـيْكَ، وَوَجَّـهْتُ وَجْـهي إِلَـيْكَ، وَأَلْـجَـاْتُ ظَهـري إِلَـيْكَ، رَغْبَـةً وَرَهْـبَةً إِلَـيْكَ، لا مَلْجَـأَ وَلا مَنْـجـا مِنْـكَ إِلاّ إِلَـيْكَ، آمَنْـتُ بِكِتـابِكَ الّـذي أَنْزَلْـتَ وَبِنَبِـيِّـكَ الّـذي أَرْسَلْـت

”Ee Allaah! Nimeisalimisha nafsi yangu Kwako, nimeyaegemeza mambo yangu Kwako, nimeuelekeza uso wangu Kwako, nimeutegemeza mgongo wangu Kwako hali ya kuwa ni mwenye kukutarajia na mwenye kukuogopa, hapana sehemu ya kukimbilia wala ya kujiokoa isipokuwa Kwako. Nimekiamini Kitabu Chako ulichokiteremsha na Nabii Wako Uliyemtuma. Akifa basi amekufa juu ya maumbile. Yafanye hayo ndio ya mwisho unayosema.”[3]

Afanye du´aa hii ndio ya mwisho anayosoma.

Pia inapendeza kwake ajilinde kwa maneno kamili ya Allaah kutokana na shari ya alichoumba mara tatu. Pia aseme:

بسم الله الذي لا يضرُّ مع اسمه شيءٌ في الأرض ولا في السماء، وهو السميع العليم

“Kwa jina la Allaah ambaye hakidhuru kwa jina Lake chochote mbinguni na ardhini Naye ni Mwenye kusikia, Mjuzi wa yote.”

mara tatu. Haya yote ni katika sababu za kujilinda.

Vilevile aseme:

اللّهُـمَّ رَبَّ السّمـواتِ وَرَبَّ العَـرْشِ العَظـيم، رَبَّنـا وَرَبَّ كُـلِّ شَـيءٍ، فالِـقَ الحَـبِّ وَالنَّـوى، وَمُـنَزِّلَ التَّـوْراةِ وَالإنْجـيلِ والفُـرْقانِ. أَعُـوذُ بِـكَ مِن شَـرِّ كُـلِّ شَـيءٍ أَنْـتَ آخِـذٌ بِنـاصِـيَتِهِ. اللّهُـمَّ أَنْـتَ الأوَّلُ فَلَـيسَ قَبْـلَكَ شَيءٌ، وَأَنْـتَ الآخِـرُ فَلَـيسَ بَعْـدَكَ شَيءٌ، وَأَنْـتَ الظّـاهِـرُ فَلَـيْسَ فَـوْقَـكَ شَيءٌ، وَأَنْـتَ الْبـاطِـنُ فَلَـيْسَ دونَـكَ شَيءٌ، اقـْضِ عَنّـا الـدَّيْـنَ وَأَغْـنِنـا مِنَ الفَـقْرِ

”Ee Allaah, Mola wa mbingu na Mola wa ’Arshi tukufu. Mola wetu na Mola wa kila kitu. Mpasuaji wa mbegu na kokwa na aliyeteremsha Tawraat, Injiyl na Qur-aan. Najilinda Kwako kutokamana na shari ya kila kitu; Wewe ndiye Mwenye kukamata utosi wake. Ee Allaah! Wewe ndiye  wa Mwanzo, hakuna kitu chochote kabla Yako. Wewe ndiye wa Mwisho, hakuna kitu chochote baada Yako. Wewe ndiye Uliye juu, hakuna kitu chochote juu Yako. Wewe ndiye Uliye karibu, hakuna kitu chochote kilichofichikana Kwako. Tulipie madeni yetu na utuepushe na ufakiri.”[4]

Haya yote ni katika mambo yanayopendekezwa mtu kuyasema anapolala.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/28-kinachofanywa-kwa-aliyeota-ndoto-nzuri-au-mbaya/

[2] al-Bukhaariy (7393) na Muslim (2714).

[3] al-Bukhaariy (6311) na Muslim (2710).

[4] Muslim (2713).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31225/ماذا-يفعل-من-راى-في-منامه-ما-يسووه
  • Imechapishwa: 14/10/2025