Atasamehewa madhambi madogo ikiwa ataendelea kufanya madhambi makubwa?

Swali: Ikiwa mtu ataendelea kufanya kufanya madhambi makubwa – je, atasamehewa madhambi madogo?

Jibu: Kama Mola wako:

إِن تَجْتَنِبُوا كَبَائِرَ مَا تُنْهَوْنَ عَنْهُ نُكَفِّرْ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَنُدْخِلْكُم مُّدْخَلًا كَرِيمًا

“Mkijiepusha madhambi makubwa mnayokatazwa Tutakufutieni madhambi yenu madogo na Tutakuingizeni katika mahali patukufu.”[1]

Kwa maana ya madhambi madogo. Hiyo ni fadhilah kutoka kwa Allaah. Lakini watu wamekhitalifiana kuhusu mpaka wa dhambi kubwa; huenda mtu akadhani dhambi ni ndogo kumbe ni kubwa. Kwa hiyo inampasa ajiepushe na madhambi yote, makubwa na madogo, kwani anaweza kuangukia katika dhambi kubwa akidhani ni ndogo.

Swali: Ikiwa ataendelea na dhambi kubwa lakini akaswali swalah zake – je, zitasamehewa dhambi ndogo?

Jibu: Hapana, hazitasamehewa. Ni sharti kujiepusha na madhambi makubwa.

[1] 04:31

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31134/هل-تكفر-الصغاىر-للمصر-على-كبيرة
  • Imechapishwa: 04/10/2025