Asli katika mambo yaliyokatazwa katika Shari´ah

Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

09- Abu Hurayra ´Abdur Rahman bin Swakhr (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Kile nilichokukatazeni kiepukeni na kile nilichokuamrisheni fanyeni kwa wingi kadiri muwezavyo… “

Hili linagusa makatazo yote, sawa ikiwa ni haramu au kimechukizwa kama tulivyotangulia kubainisha. Asli ya mambo aliyokataza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ikiwa ni katika mambo ya ki-´ibaadah inakuwa ni haramu. Na ikiwa ni katika mambo ya kidesturi inakuwa imechukizwa. Kwa msemo mwingine ni kwamba, kunapokuja makatazo katika jambo miongoni mwa mambo ya ´ibaadah inakuwa ni kwa njia ya uharamu. Kwa kuwa asli katika mambo ya ´ibaadah ni kukomeka (Tawqiyf). Na kukija makatazo katika jambo miongoni mwa mambo ya adabu, asli ni kwamba inakuwa ni kwa njia ya machukizo…

Mfano wa hilo ni maamrisho ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mtaje Allaah! Kula kwa mkono wa kulia na kula mbele yako.” (al-Bukhaariy (5376))

Wanachuoni wengi wanaonelea kuwa kula kwa mkono wa kulia imependekezwa na kula kwa mkono wa kushoto imechukizwa. Wapo pia waliosema kuwa ni haramu kula kwa mkono wa kushoto. Haya ni mambo waliyotofautiana kwayo wanachuoni.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 181-183
  • Imechapishwa: 17/05/2020