Swali: Ni ipi hukumu ya kuondosha nywele za mikononi na miguuni kwa kuwa ni jambo lililoenea kwa wanawake wengi?

Jibu: Nywele za mwili ziko aina mbili:

1- Kuko ambazo ni wajibu kuziondosha; kama nywele za makwapani na nywele za sehemu za siri. Hili ni kwa mwanaume na kwa mwanamke. Vilevile kukata masharubu kwa mwanaume.

2- Nywele ambazo ni wajibu kuzibakiza; kope, nyusi, ndevu kwa mwanaume.

Kuna nywele ambazo zimenyamaziwa na imeruhusiwa; hizi ni kama nywele za miguuni na kwenye muundi. Ni sawa kuziondosha. Lakini hata hivyo kuziacha ni bora zaidi kwa kuwa akiziondosha ni jambo linaweza kumuudhi na zikawa zinakuwa kwa haraka. Hivyo akiziacha ni bora zaidi. Nywele kama hizi yameruhusiwa yote mawili, sawa kuziondosha na kuziacha.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://ar.islamway.net/lesson/138827/%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B1%D8%A3%D8%A9-%D8%AD%D9%82%D9%88%D9%82-%D9%88%D9%88%D8%A7%D8%AC%D8%A8%D8%A7%D8%AA?ref=s-pop
  • Imechapishwa: 24/09/2020