Anayetamka shahaadah kwa ajili ya kuepuka kifo

Swali: Ni ipi hukumu ikiwa tutamuona kafiri akifanya kitendo cha yule mtu aliyekuwa na Swahabah, kisha akataka kuokoka akasema ”Laa ilaaha illa Allaah” na Allaah anajua zaidi kuhusu nia yake?

Jibu: Hatauawa. Akiisema na hakuwa akiisema kabla, basi inatakiwa kuchunguzwa hali yake. Hata kama ikidhaniwa kuwa aliisema kwa kujiepusha na kuuawa, kama alivyokataa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) maneno ya Usaamah alipomwambia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Aliisema kwa kujikinga.” Ndipo Mtume akamwambia: ”Je, uliupasua moyo wake?”

Basi ikiwa hakuwa akiisema kabisa kisha akaisema, inatakiwa asichukuliwe hatua hadi hali yake ichunguzwe.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31462/ما-العمل-تجاه-من-قال-لا-اله-الا-الله-تعوذا
  • Imechapishwa: 24/10/2025